Lamentations 2:3-5


3 aKatika hasira kali amevunja
kila pembe
Pembe inawakilisha nguvu; pia 2:17.
ya Israeli.
Ameuondoa mkono wake wa kuume
alipokaribia adui.
Amemteketeza Yakobo kama moto uwakao
ule uteketezao kila kitu kinachouzunguka.


4 cAmeupinda upinde wake kama adui,
mkono wake wa kuume uko tayari.
Kama vile adui amewachinja
wote waliokuwa wanapendeza jicho,
amemwaga ghadhabu yake kama moto
juu ya hema la Binti Sayuni.


5 dBwana ni kama adui;
amemmeza Israeli.
Amemeza majumba yake yote ya kifalme
na kuangamiza ngome zake.
Ameongeza huzuni na maombolezo
kwa ajili ya Binti Yuda.

Copyright information for SwhKC